Ijumaa , 6th Mar , 2020

Afisa Mhamsasishaji na Msemaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amewapa mashabiki wa klabu hiyo kitu cha kutamba nacho siku zote kutokana na kile walichokifanya.

Antonio Nugaz

Nugaz amesema hayo kuelekea mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba unaotarajiwa kupigwa Jumapili hii, Machi 8, 2020 katika uwnja wa taifa.

Amesema kuwa mashabiki wa Yanga wana hadhi kubwa kuliko timu yoyote Tanzania, kuwa timu hiyo ina hadhi ya ubingwa wa kihistoria na hadhi ya kubeba vikombe vingi vya Ligi Kuu kuliko timu nyingine yoyote.

"Tembea kifua mbele na kibingwa, usitishwe na usiogopeshwe na fahamu hadhi yako ni kubwa. Bila makando kando sisi lazima tushinde, tunashinda popote pale na muda wowote", amesema Nugaz.

Kuelekea mchezo huo, Nugaz amesema wadhamini wa klabu, GSM wameahidi kutoa Sh. milioni 200 endapo watafanikiwa kushinda mchezo huo Jumapili.