Jumatatu , 9th Jan , 2017

Mesut Ozil yuko tayari kusaini mkataba mpya na Arsenal lakini anataka kujua kama meneja Arsene Wenger atabaki kwenye klabu hiyo baada ya mwisho wa msimu huu.

Ozil (kushoto) na Wenger kwenye mazoezi

 

Mkataba wa Wenger unamalizika mwishoni wa msimu huu wakati mikataba ya Ozil na mchezaji mwenzake Sanchez inamalizika baada ya miezi 18.

Ozil amesema kuwa anafurahi sana kubaki kwenye klabu ya Arsenal na amewaambia viongozi wa timu hiyo kuwa angependa kuongeza muda wa mkataba wake.

"Nina furaha sana ndani ya Arsenal na nimeiacha klabu itambue hilo kwamba nipo tayari kusaini mkataba mpya."Alisema Ozil akiongea na waandishi wa habari za michezo za Ujerumani.

"Mashabiki wanataka nibaki na sasa ni uamuzi wa klabu.

"Wanajua kwamba nipo hapa kwa sababu ya Arsene Wenger. Yeye ndiye aliyenileta na yeye ndiye anayeamini nilichonacho. Klabu pia inajua kwamba nataka kuwa muwazi na kile meneja anataka kufanya."