Tyson Fury baada ya kushinda mkanda wa ubingwa wa uzito wa juu WBC kwa kumpiga Deontay Wilder Februari 2020 nchini Marekani.
Kauli ya Warren imekuja baada ya Fury kusaini mkataba mnono na ESPN uliomlazimu mapambano yake manne yafanyike nchini Marekani likiwemo lile la mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare na Deontay Wilder mwaka uliopita.
Fury ambaye mara yake ya mwisho pambano lake kufanyika nchini England ilikuwa ni mwaka 2018, anatazamiwa kupambana kati ya Oleksander Usyk au Anthony Joshua licha ya pambano la Joshua kuonekana kuwa hai zaidi.






