Jumamosi , 9th Oct , 2021

Bingwa wa tennis wa US Open, Muingereza Emma Raducanu amefungwa seti 6-2, 6-4 na Aliaksandra Sasnovich na kutolewa kwenye hatua ya mzunguko wa pili wa mashindano ya BNP Paribas Open yanayofanyika Indian Wells nchini Marekani.

(Emma Raducanu akiinama kichwa chini baada ya kufungwa seti zote na Sasnovich kwenye BNP Paribas Open jioni ya leo Oktoba 9, 2021 nchini Marekani)

Raducanu anayeshikilia nafasi ya 22 kwa ubora duniani kwa upande wa Wanawake amesema Sasnovich alikuwa bora sana ndiyo maana aliweza kuibuka na ushindi huo.

“Nafikiri Aliaksandra alicheza mchezo mzuri sana. Alikuwa bora kuliko mimi leo, alistahili kupata ushindi. Mimi ni mtu ambaye kitu kikitokea kimetokea kwahiyo ninaweza kujifunza na kujitoa ushamba”.

“Kwenye kufungwa kokote kuna kuwa na dis-appointment. Sikwenda kucheza kwa kujipa presha zaidi ya kushinda kwasababu akili yangu bado haina uzoefu kwahiyo nimepokea kilichotokea” alimalizia hivyo Raducanu.

Kipigp hiko kimemfanya Raducanu mwenye umri wa miaka 18 kushindwa kupata ushindi wake wa 11 mfululizo tokea afungwe mara ya mwisho Agosti 22 mwaka huu.

Ushindi kwa Sasnovich anayeshika nafasi ya 100 duniani acheze na bingwa mara mbili wa Grand Slam, Simona Halep kwenye mzunguko watatu wakati Leyla Fernandez wa Canada makamu bingwa wa US Open ametinga mzunguko watatu baada ya kumfunga Alize Cornet wa Ufaransa kwa 6-2&6-3