Jumapili , 16th Mei , 2021

Klabu ya Leicester City imetwaa ubingwa wa kombe la FA usiku jana kwa kuifunga Chelsea bao 1-0 katika uwanja wa Wembley, mchezo ambao ulioudhuriwa na mashabaki 20,000 kwa mara ya kwanza tangu janga la Corona lilipoingia.

Kasper Schmeichel na Wesley Morgan akishangalia Ubingwa wa FA

Kasper Schmeichel golikipa wa Leicester City aliandikisha rekodi nyingine nzuri ya kuvutia baada ya kutwaa ubingwa huo, kwa kuwa mchezaji wa pili yeye na baba yake mzazi Peter Schmeichel kutwaa ubingwa huo 1994 akiwa na Manchester United. Wengine ni wengine ni Ian Wright akiwa na Arsenal na mwanae Shaun Wright akiwa na Manchester City.

Rekodi nyingine iliwekwa na Jimie Vardy kushiriki michuano hii katika ngazi zote 13 toka zile za awali kabisa akiwa na vilabu vidogo alivyoanzia mwaka 2012 na hatimaye kucheza fainali na kutwaa ubingwa,FA mwaka 2021 Uingereza huchezwa na timu 736.

Aiyawatt Srivaddhnaprabha mtoto wa aliyekuwa mmiliki wa Leicester City marehemu Vichai Srivaddhanaprabha ambaye alifariki dunia mwaka 2018 kwa ajali ya helkopta ameendeleza pale alipoishia baba yake ambaye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa EPL msimu wa 2015/2016.

Wakati Leicester City akitwaa ubingwa wao wa kwanza,wanakuwa mabingwa wa 44 tangu michuano hiyo imeanzishwa mwaka 1871-72.

Kelechi Iheanacho na Wilfrid Ndidi kutoka klabu ya Leicester City wanakuwa Wanaigeria wa 8 na 9 kutwaa ubingwa wa FA wengine ni Daniel Amokachi, Nwanko Kanu, John Utaka, Mikael Obi, Victor Moses, Alex Iwobi, Winfred Ndidi Kelechi Iheanacho.