Jumamosi , 11th Jul , 2020

Nusu fainali ya kwanza ya Azam Sports Federation Cup, inachezwa leo Saa 9:00 Alasiri uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. 

Kikosi cha Namungo FC

Katika mchezo huo timu pekee ya ligi daraja la kwanza iliyosalia katika michuano hiyo ni Sahare All Stars ya Tanga na watakuwa wenyeji wa Namungo fc ya mkoani Lindi.

Katika hatua ya robo fainali Sahare waliitoa Ndanda fc ya Mtwara kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Katika safari ya Sahare mpaka wanafika nusu fainali waliitoa Njombe mji katika mzunguko wa 64, hatua ya 32 bora waliitoa Mtibwa sugar na hatua ya 16 bora waliiondoa Panama Fc.

Namungo walikata tiketi  ya kucheza nusu fainali baada ya kuifunga Alliance fc ya Mwanza mabao 2-0 kwenye mchezo wa robo fainali. Namungo waliitoa Green Worrios katika mzunguko wa 64, hatua ya 32 bora waliifunnga Biashara united na wakaitoa Mbeya City katika hatua ya 16 bora.

Mshindi wa nusu fainali hii ya kwanza atacheza na mshindi wa nusu fainali ya pili itakayochezwa kesho kati ya Simba dhidi ya Yanga.