Ripoti ya ajali iliyomuua Kobe Bryant imetoka

Jumamosi , 16th Mei , 2020

Ripoti ya post-mortem ya ajali ya Helikopta iliyoua watu 9 akiwemo nguli wa mchezo wa Kikapu Kobe Bryant na mwanaye wa kike Gianna, imetoka na imeeleza kuwa kukosekana kwa hewa, mwanga na mazingira magumu ilipoangukia ndio sababu ya wote kupoteza maisha.

Picha ya eneo la ajali pamoja na Kobe Bryant na binti yake Gianna.

Kitaalamu tukio hilo linaitwa (blunt force trauma).

Ripoti hiyo yenye kurasa 180, ilitolewa jana Mei 15, 2020 na Mamlaka za uchunguzi wa afya jijini Los Angeles (Los Angeles County Medical Examiner-Coroner) na imeeleza kuwa rubani ambaye alikuwa na miaka 50 hakuwa ametumia kilevi au madawa.

Ajali hiyo iliyotokea Januari 26 huko California ilichukua uhai wa watu 9 ambao ni Alyssa Altobelli, John Altobelli, Keri Altobelli, Sarah Chester, Payton Chester, Christina Mauser, Kobe Bryant, Gianna Bryant na rubani Ara Zobayan.

Pia ripoti imeeleza kuwa rubani Mr Zobayan alikuwa kwenye afya na hali imara tu na ndege ilikuwa bado na uwezo wa kupaa masaa 8,200.

Aidha changamoto nyingine ambayo imeelezwa kusababisha ajali hiyo ni mawingu pamoja na mvua nyepesi (fog) ambazo zilisababisha zaidi ya simu 911 zilizopigwa kati ya rubani na kituo cha kusimamia mwenendo wa ndege.