Jumamosi , 15th Dec , 2018

Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani, leo atakuwa jukwaani akiitazama timu yake ya Yanga ikicheza na Ruvu Shooting kwenye ligi kuu soka Tanzania bara kwenye uwanja wa taifa.

Kelvin Yondani

Beki huyo mkongwe nchini anatumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano hivyo atalazimika kukosa mchezo huo, ambao unaweza kuwapa nafasi Yanga ya kuendelea kutanua wigo wa alama na wapinzani wao wa karibu Azam FC na Simba.

Mbali na Yondani mchezaji mwingine ambaye kocha Mwinyi Zahera amethibitisha kuwa hayuko fiti kwaajili ya mchezo huo ni Raphael Daudi ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

Kocha huyo pia amebainisha kuwa mshambuliaji Ibrahim Ajibu yupo fiti kwa mchezo baada ya kurejea kambini Desemba 13 akitokea kwenye msiba. 

Kiungo kutoka Zanzibar Feisal Salum naye ameungana na timu juzi akitokea kwao, ambako alikwenda kwenye msiba wa dada yake, hivyo atakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

Yanga wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 41, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 40 na Simba 27.