Jumamosi , 8th Aug , 2020

Klabu ya soka ya Juventus imetangaza kumfuta kazi kocha wake Maurizio Sarri ambaye amedumu kwa mwaka mmoja pekee na miamba hiyo ya nchini Italia.

Aliyekua kocha wa Juventus , Maurizio Sarri katika picha akiwa na taji alilotwaa na miamba hiyo ya Italia.

Sarri mwenye umri wa miaka 61, alijiunga na Chelsea msimu uliopita na kuiongoza Juventus kutwaa Ubingwa wa Sere A kwa mara ya tisa mfululizo ingawa timu hiyo imeshindwa kuonyesha kiwango bora kwenye michezo ya mwisho wa msimu .

Inatajwa kuwa miongoni mwa sababu kubwa zilizopelekea kutimuliwa kazi kwa kocha huyo ni kutokana na kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Lyon ya Ufaransa.

Kocha huyo alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia Juventus lakini inaonekana hajatimiza malengo ya timu ambayo ililenga zaidi kufanya vyema nje ya Italia.