Jumanne , 11th Dec , 2018

Klabu ya soka ya Simba kesho inatarajiwa kuondoka nchini kuelekea nchini Zambia ambako itacheza mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika hatua ya kwanza dhidi ya Nkanda Reds ya huko.

Wachezaji wa Simba

Msafara huo wa Simba utaongozwa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini (TFF), Francis Ndulane.

''Msafara utakuwa na wachezaji 20, watu 6 kutoka benchi la ufundi pamoja na viongozi watatu wa klabu'', amesema Manara.

Aidha Manara ameongeza kuwa msafara huo utaondoka saa 10:00 alfajiri kwa ndege ya moja kwa moja hadi Addis Ababa Ethiopia kisha kuunganisha hadi Ndola Zambia na baadaye mjini Kitwe ambako mchezo huo utapigwa.

Nkana Red Devils walipata nafasi ya kushiriki klabu bingwa Afrika baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi yao wakiwa nyuma ya Zesco United msimu uliopita.