Alhamisi , 13th Aug , 2020

Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza Tamasha la Siku ya Simba(Simba Day) ambalo hufanyika kila mwaka ambapo kwa mwaka huu litafanyika Jumamosi ya Agosti 22 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba , Haji Manara (Pichani)

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema Timu yao imekuwa na utaratibu wa kufanya Tamasha hilo ambalo hutumia kwa kutambulisha wachezaji watakao watumia kwa ajili ya msimu mpya wa ligi pamoja na jezi.

Manara amesema ''Simba Day itatanguliwa na Wiki ya Simba ambayo imepewa jina la 'CHAMPIONS WEEK, ANOTHER LEVEL ambayo itadhaminiwa na SportPesa ambao ndio wadhamini wakuu wa klabu.

Ndani ya Simba wiki kutakuwa na matukio makubwa kama kuzindua logo mpya ya klabu na jezi mpya za msimu.

Kwa siku ya kesho ambayo ni Agosti 14,Simba watafanya usafi kwenye fukwe za Coco Beach na kujitolea damu.

MAMBO MAKUU MATATU YATAKAYOFANYIKA KESHO.

1-Mchana kuzindua Logo mpya iliyoboreshwa .

2.Jezi mpya za msimu mpya wa mwaka 2020/ 2021.

3.Utambulisho wa wachezaji wapya wa msimu 2020/ 2021.

4.Watafanya usafi maeneo ya Salenda Bridge.