Jumapili , 20th Mei , 2018

Kaimu Rais ya wa klabu ya Simba Salum Abdallah amethibitisaha kwamba kuanzia msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara 2018/209 klabu hiyo itaanza kutumia uwanja wake wa mazoezi.

Kaimu Rais huyo amesema hayo leo Mei 20, 2018 katika mkutanao mkuu wa dharura wa klabu hiyo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa kwa msimu ujao Simba itakuwa ni timu isiyokamatika kwa maendeleo

“Msimu ujao Simba haitashikika, mnaweza kuona mambo haya yamechelewa kidogo lakini tulikuwa tunajua kiu ya wanasimba ilikuwa ni ubingwa, sasa ubingwa tumeshapata, tunaenda kuleta maendeleo katika klabu yetu, msimu ujao timu itafanya mazoezi katika uwanja wetu” amesema Abdallah 

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikua waziri wa habari, utamadunu sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe ambaye aliunga mkono mabadirko hayo kwa niaba ya serikali  na kuipongeza timu ya simba na kuomba klabu nyingine kufuata mfano kwasababu mabadiriko hayazuiliki.

Katika mabadiriko hayo wanachama wa Simba sasa watakuwa na uwezo wa kumiliki hisa 51% na mmiliki mwenye hisa nyingi ambaye ni Mohamed Dewji atamiliki 49% ya hisa katika jina la kampuni litakalojulikana kama Simba Sports Club Company Limited.