timu ya Taifa ya vijana ambayo msingi wake ni michuano hii
Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano haya, leo juni 10 2020 ambapo ndipo yanafunguliwa rasmi , kutakuwa na michezo miwili tu ,wa kwanza majira ya Saa 1:00 Usiku ni JKT Tanzania dhidi ya Mwadui na baadaye Saa 3:00 Usiku ni Simba dhidi ya Yanga katika uwanja wa Chamazi.
Mashindano haya yapo kwenye makundi ya mawili, yenye timu nne kila moja, ambapo timu mbili za juu kwenye kila kundi zitasongambele katika hatua ya nusu fainali. Makundi hayo ni,
KUNDI A KUNDI B
1 Simba SC 1 Tanzania Prisons
2 Yanga 2 Kagera Sugar
3 JKT Tanzania 3 Azam FC
4 Mwadui 4 Mtibwa Sugar