Simba yaanza usajili rasmi

Jumatatu , 10th Jun , 2019

Klabu ya Simba imeanza rasmi usajili kuelekea msimu mpya wa ligi kuu 2019/20 kwa kutangaza usajili wa nahodha wa klabu hiyo, John Bocco.

John Bocco akisaini mkataba

John Bocco amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba kuanzia msimu ujao, ikiwa ni baada ya kuonesha ubora mkubwa katika msimu uliomalizika.

Taarifa hiyo imetolewa kupitia kurasa rasmi za klabu hiyo, ikiwemo Twitter.

Katika msimu wa 2018/19, John Bocco ameifungia Simba mabao 16 ya ligi.