Jumatano , 13th Feb , 2019

Baada ya jana kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mechi ya 4 ya kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya soka ya Simba itakuwa na ratiba ngumu katika mechi zake zijazo.

Kocha wa Simba Patrick Aussems

Baada ya mechi ya jana, Simba imeanza maandalizi tayari kwa mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Yanga ambao utapigwa 16/02/2019 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Baada ya hapo Simba itasafiri Jumapili kwenda Arusha ambapo itafanya mazoezi kwa siku moja kabla ya mechi yake dhidi ya African Lyon itakayopigwa 19/02/2019.

Kisha itarejea Dar es salaam na kujianda kwa siku moja kisha kushuka dimbani 22/02/2019 dhidi ya Azam FC. Baada ya mchezo huo kesho yake inasafiri kwenda Iringa na inakuwa na siku 2 za mazoezi ambapo itacheza 26/02/2019 dhidi ya Lipuli FC.

Kisha itaunganisha kwenda Shinyanga na itakuwa na siku 2 tu za mazoezi kabla ya 03/03/2019 kuivaa Stand United.

Baada ya mechi hiyo Simba itarudi Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda Algeria 06/03/2019 ambapo itasafiri kwenda kucheza na JS Saoura Machi 9/2019.

Simba sasa inashika nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na alama 6 nyuma ya Al Ahly yenye alama 7 huku JS Saoura wakishika nafasi ya tatu wakiwa na alama 5 na AS VItal wakishika mkia wakiwa na alama zao 4.