Stars kupaa kesho AFCON, nyota wake aachwa

Alhamisi , 6th Jun , 2019

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kupaa kesho kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kumalizia kambi, kabla ya michuano ya mataifa ya Afrika AFCON kutimua vumbi nchini humo.

Taifa Stars

Kikosi hicho kinatarajia kuagwa hii leo na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kwenye kambi yao jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo hazijathibitishwa, zinaeleza kwamba kikosi cha Stars kitaondoka nchini bila ya beki wake kisiki, Shomari Kapombe ambaye hivi karibuni ameshika kasi katika vichwa vya habari kutokana na sintofahamu ya majeraha yanayomkabili.

Shirikisho la Soka nchini, TFF lilitoa taarifa kuwa mchezaji huyo amejitonesha majeraha yake, hivyo kuna wasiwasi wa nafasi yake katika kikosi cha taifa. Taarifa hiyo ilikanushwa na mchezji mwenyewe, huku akisisitiza kuwa yeye yuko fiti kucheza.