Stori ya ndani kuhusu nyota wanne wa Tottenham

Jumanne , 30th Apr , 2019

Kuelekea nusu fainali ya kwanza ya Klabu bingwa Ulaya leo kati ya Tottenham na Ajax, hawa ndio nyota wanne waliochezea hizi timu mbili lakini kwasasa wapo Tottenham.

Wachezaji Christian Eriksen, Davinson Sánchez, Jan Vertonghen na Toby Alderweireld.

Moja ya nyota hao ni kiungo Christian Eriksen ambaye yeye alianza soka lake katika klabu ya Ajax mwaka 2010 hadi 2013 ambapo alitimkia katika klabu ya Tottenham.

Eriksen ametumia uzoefu wake wa kuwa na Ajax kuwatahadharisha wenzake wa Tottenham kuwa wapinzani wao hawana uoga na timu yoyote na huo ndio utamaduni wao wa kucheza soka la kujiamini wakiwa nyumbani ama ugenini.

Wachezaji wengine ambao wapo Tottenham na walianzia Ajax ni Davinson Sánchez  mwaka 2016 hadi 2017, Jan Vertonghen 2006 hadi 2012 na Toby Alderweireld 2004 hadi 2008.

Mchezo wa leo unapigwa kwenye uwanja wa Tottenham kabla ya mkondo wa pili kupigwa huko Uholanzi. Katika hatua ya mtoano Tottenham waliitoa Tottenham na robo fainali wakaitoa Man City. Ajax walizitoa Real Madrid na Juventus.