Alhamisi , 24th Sep , 2020

Luis Suarez amejiunga rasmi na Atletico Madrid akitokea katika timu ya Barcelona aliyojiunga nayo mwaka 2014 mara baada ya kombe la dunia nchini Brazil kumalizika , huku ada ya uhamisho wake ikitajwa kuwa paundi milion 5.5

luis Suarez akishangilia moja ya magoli aliyoyafunga akiwa Barcelona

Suarez ni moja ya washambuliaji bora duniani, kwa miaka 10 hii ameonesha makali yake akiwa na  vilabu vya Ajax  ya  Uholanzi, Liverpool na Barcelona.

Akiwa na Barcelona,  alidumu kwa miaka sita na kufanikiwa  kutwaa kombe la Laliga mara 4, kombe la Mfalme mara 4, kombe la Hispania  mara 2, kombe la Mabingwa Ulaya  mara 1  na kombe la  FIFA  la dunia kwa ngazi ya vilabu   mara  1

UBORA WA SUAREZ UPO WAPI ?
Suarez  ni moja ya wachezaji wanaoweza kutengeneza nafasi za kufunga  kwa wenzake, na pia  ana uwezo wa kufunga  yeye mwenyewe, kwa   mashuti mazito.

Anafunga magoli kwa aina zote zinazohitajika kwenye soka, ni mzuri kwa kwa kutumia kichwa  na pia mzuri kwa matumizi ya miguu yote miwili katika kufunga , jambo lililompa uwezo wa kuifungia  Barcelona  magoli 198  katika  michezo 283.

CHANGAMOTO ZAKE

Matatizo  ya Suarez ni ukorofi kwa wachezaji  wenzake  ikiwemo matukio ya kuwang'ata  kama Othman  Bakkal, Branislav Ivanovic ,Georgio Chiellin pia ana tuhuma  za ubaguzi wa rangi kwa wachezaji weusi  hasa kisa chake  dhidi ya mchezaji wa zamani wa Manchester Utd Patrice  Evra .