TFF yafungukia mchezo wa Gor Mahia dhidi ya Yanga

Jumatano , 13th Jun , 2018

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa (CAF) limetaja waamuzi kutoka nchini Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani Julai 18,2018.

Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kusemma kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba 2 Suleiman Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.

Mtathmini waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo Nomsa Jacobeth Mahlangu.

Aidha, mchezo wa marudiano kwa timu hizo unatarajiwa kuchezwa Juli 29, 2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius. 

Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Cauvelet Louis Ralph Fabian,Mwamuzi msaidizi namba 2 Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.

Kwa upande mwingine, Kamishna wa mchezo huo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru Sarkintudu Jibr