Jumatano , 13th Feb , 2019

Shirikisho la soka nchini (TFF), kupitia kwa Idara ua Ufundi limemleta mkufunzi wa tiba ya viungo kwa wanamichezo Johnny Wilson kutoka Englanda kwa ajili ya kutoa kozi kwa madaktari wa timu za ndani.

Mkufunzi Johnny Wilson akitoa maelekezo.

Akiongea leo, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Ammy Ninje ameweka wazi kuwa kozi hiyo imeanza leo Jumatano Februari 13, 2019 kwenye Taasisi ya mifupa Muhimbili (MOI) ikishirikisha madaktari wa timu mbalimbali.

''Kozi imeanza leo na wamejitokeza madaktari zaidi ya 50, lakini kutakuwa na kozi tofauti tofauti ndani ya siku 4 hivyo ni mwanzo mzuri wa kuboresha tiba kwa wachezaji'', amesema Ninje.

Aidha mkurugenzi huyo amesema hawataishia hapa bali zoezi hili litakuwa endelevu ili kuhakikisha watanzania wengi wanafaidika na kusaidia kuboresha maeneo husika katika soka letu.