Jumatatu , 9th Mar , 2020

Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF limetangaza mahudhurio na mapato yaliyopatikana katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba, Jumapili Machi 8, 2020.

Uwanja wa taifa kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Simba

Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa taifa na kumalizika kwa Simba kukubali kichapo cha bao moja, ikiwa ni kichapo cha kwanza kutoka kwa mahasimu wao katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Jumla ya watazamaji elfu hamsini na tisa na mia tatu ishirini na tano (59325) walihudhuria mchezo huo na kuingiza jumla ya Shilingi milioni mia tano na arobaini na tano laki nne na ishirini na mbili elfu (545,422,000).

Kwa mujibu wa sheria mpya za mapato ya uwanjani za Bodi ya Ligi, baada ya kodi na makato ya uwanja, mapato yote yanayobakia yanakwenda kwa timu mwenyeji wa mchezo huo ambao ni Yanga.