Jumatatu , 21st Sep , 2020

Kiungo mpya wa Liverpool Thiago Alcantara ameweka rekodi ya kupiga pasi nyingi kwenye ligi kuu England EPL ndani ya dakika 45, amepiga pasi 75 zilizokamilaka kwenye mchezo dhidi ya Chelsea Liverpool ikishinda 2-0.

Alcantara ameweka rekodi ya kupiga pasi 75 zilizokamilika ndani ya daika 45 kwenye ligi kuu England EPL

Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania alikamilisha usajili wa kujiunga na Liverpool siku ya ijumaa kwa ada ya uhamisho ya zaidi ya billion 74 kwa fedha za kitanzania akitokea Bayern Munich ya Ujerumani, lakini kocha Jurgen Klopp alimjumuhisha kiungo huyo kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Jijini London kwenye mchezo dhidi ya Chelsea uliochezwa jana Jumapili.

Thiago alianzia benchi katika orodha ya wachezaji wa akiba na dakika ya 45 kipindi cha pili aliingia kuchukua nafasi ya nahodha Jordan Henderson ambaye alipata majeruhi. Kilichofata ilikuwa kiwango bora kutoka kwa Alcantara akaonyesha thamani yake kwenye kikosi cha kocha Jurgen Klopp na kutuonyesha kwa nini Liverpool imemsajili.

Licha ya kucheza dakika 45 tu kiungo huyo wa zamanai wa Barcelona na Bayern Munich alipiga pasi 75 zilizokamlika ikiwa ni nyingi zaidi kuliko mchezaji yeyote wa Chelsea ikijumuisha na wale waliocheza dakika 90.

Hii ni rekodi kwenye ligi kuu England EPL kwa mchezaji kupiga pasi nyingi 75 zilizokamilaka chini ya dakika 45 tangu mwaka 2003.

Wakati Thiago Alcantara akiwa anatamba kwenye kiungo cha majogoo wa Merseyside, Liverpool walishinda mabao 2-0 maboa yote yalifungwa na Sadio Mane ambaye alifunngwa bao la kwanza kwa kichwa akimalizia mpira uliopigwa na Roberto Firmino dakika ya 50 na dakika 4 baadaye akafunga tena baada ya golikipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga kufanya makosa kwenye lango lake.