Jumamosi , 20th Jul , 2019

Klabu ya soka ya Alliance FC, ya jijini Mwanza imetangaza benchi lake kamili litakaloongoza msimu huo ambapo imeingia mkataba wa miaka na kocha Athumani Bilali.

Bilali ambaye ni mwalimu mzoefu katika ligi ya Tanzania amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumiakia timu hiyo ambayo itakuwa inacheza ligi kwa msimu wake wa pili.

''Sisi kama Alliance tumemuamini na tunaimani naye kubwa kwani hatuangalii vile alivyoanguka huko alikotoka bali tunaangalia kwanini alianguka na tufanye nini ili asianguke tena'', wamesema Alliance.

Benchi kamili la Alliance.
Kocha mkuu - Athumani Bilali
Kocha msaidizi - Kessy Mziray
Kocha msaidizi - Daddy Gilbert
Kocha wa makipa - Hussein Thade
Daktari wa timu - Abel- shindika
Mtunza vifaa - Josephat Munge

Timu hiyo imeeleza kuwa itaanza mazoezi rasmi Jumatatu Julai 22, 2019 na wataanza kwa semina kisha wachezaji watapimwa afya na baadaye watapewa vifaa vya kufanyia mazoezi na kuanza mazoezi.