Zambia ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Misozi Zulu katika dakika ya 44 ya mchezo huo.
Twiga Stars waliongeza makali katika kipindi cha pili na kufanikiwa kuandika mabao mawili ya haraka haraka yali yofungwa na Sherder Boniface ambapo mpaka dakika ya 59 walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Gracer Chanda aliisawazishia Zambia kunako dakika ya 69 na kurudisha matumaini kwa Zambia ambapo hata hivyo Asha Rashid aliiongezea Twiga Stars bao la tatu kunako dakika ya 77 kwa shuti la mbali kabla ya nahodha Sophia Mwasikili kuandika bao la nne katika dakika ya 89.
Zambia ilifuzu kuelekea kwenye fainali za mataifa ya Afrika mwaka jana baada ya kuifunga Twiga Stars lakini mara hii watakuwa na wakati mgumu kuelekea katika fainali za michuano ya All African Games Congo Brazzaville.
Mechi ya marudiano kati ya Twiga Stars na Zambia itachezwa wiki mbili zijazo ambapo Zambia watakuwa wageni Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.






