Jumanne , 12th Nov , 2019

Uongozi wa klabu ya Yanga umeanza rasmi kutekeleza ahadi ya kudhibiti mapato ya klabu hiyo hasa kutokana na mauzo ya jezi.

Jezi feki za Yanga zilizokamatwa leo, Dar es Salaam

Viongozi wa Yanga wakiongozwa na Msemaji na Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, ambapo wametembelea katika maduka mbalimbali ya Kariakoo, wakiungana na mtengenezaji na msambazaji wa jezi hizo, kampuni ya GSM.

"Hii tumeifanya leo pale Kariakoo mtaa wa Aggrey na Congo, baada ya kupata taarifa nikiwa ofisini na nilipigiwa simu na maintelijensia wa Yanga. Tumefanikiwa kukamata jezi feki za msimu huu na zile za zamani na mwenye duka ameonesha ushirikiano na sisi", amesema Antonio Nugaz.

"Tunawaomba wanachama na mashabiki wa Yanga kununua jezi 'origianal' za Yanga, jezi ya Yanga haitandikwi chini wala haitundikwi kwenye mti. Nunua kutoka kwa mawakala na wauzaji waliothibitishwa, isiwe mnalalamika tu kwamba Dante halipwi wakati pesa wanaochukua watu wachache ", ameongeza.

Msemaji wa Yanga amesema zoezi hilo litakuwa endelevu nchini ili kuhakikisha klabu inafaidika kutoka kwenye mauzo ya jezi halisi zinazozalishwa na kampuni iliyopewa kazi hiyo.