Alhamisi , 14th Feb , 2019

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema uwanja mkuu wa taifa utafungwa kwa muda ili kupisha maandalizi ya fainali za michuano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17.

Uwanja wa taifa

Akiongea leo Februari 14, kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya shirikisho la soka nchini (TFF), Mwakyembe amesema ili eneo la kuchezea na miundombinu mingine ya uwanja huo iwe kwenye ubora ni lazima ipunguziwe majukumu.

''Tutaufunga uwanja wetu wa taifa kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya mashindano kuanza ili kuweka sawa ubora wa miundombinu yake kwaajili ya michuano hiyo mikubwa Afrika'', amesema.

Michuano hiyo inaanza 14–28 April 2019 hivyo uwanja wa taifa utafungwa kuanzia Machi 14.

Kwasasa uwanja huo unatumika kwa mechi za ligi kuu soka Tanzania bara zinazohusisha vilabu vya Yanga, Simba pamoja na Azam FC inapocheza na timu hizo. Pia Simba inautumia katika michuano ya klabu bingwa Afrika.