Jumatano , 4th Mar , 2020

Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya 'Harambee Stars' na kiungo wa Tottenham Hotspurs, Victor Wanyama, ameachana na klabu hiyo.

Victor Wanyama

Wanyama alisajiliwa na Spurs kutokea Southampton mwaka 2016 na kufanikiwa kuichezea michezo 69, akifunga mabao sita na mafanikio makubwa aliyoyapata ni kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu nchini Uingereza pamoja na kikosi chake kufika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya msimu uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Wanyama ameandika ujumbe wa kuishukuru Spurs kwa kipindi chote cha miaka minne alichohudumu na kikosi hicho.

Amejiunga na klabu ya Montreal Impact inayoshiriki Ligi kuu ya nchini Marekani (MLS), chini ya mchezaji nguli wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry.