Virusi vya Corona vyatibua mechi Man City, Arsenal

Jumatano , 11th Mar , 2020

Mchezo wa Ligi ya Uingereza uliotakiwa kuchezwa leo kati ya Manchester City na Arsenal umeahirishwa kufuatia hofu ya virusi vya Corona.

Sergio Aguero na Pierre-Emerick Aubameyang

Hofu hiyo imekuja baada ya taarifa kuwa mmiliki wa klabu ya Olympiacos ya nchini Ugiriki, Evangelos Marinakis kukumbwa na virusi hivyo, baada ya mchezo wa Europa League kati ya Arsenal na Olympiacos uliopigwa wiki mbili zilizopita.

Baadhi ya wachezaji wa Arsenal walikutana na mmiliki wa klabu ya Olympiacos baada ya mchezo huo kumalizika na baadaye alikutwa na virusi hiyo baada ya kufanyiwa vipimo na kuzua hofu kuhusu usalama wa baadhi ya wachezaji wa klabu ya Arsenal kuelekea kwenye mchezo.

Wachezaji wa Arsenal ambao wanashukiwa kukutana na bosi huyo, wamepewa ruhusu ya kubaki nyumbani kwa muda wa siku 14 na kujiepusha na mgusano na watu, huku uongozi wa Arsenal ukimuombea bosi huyo kurejea kwenye ubora wake.

Wachezaji wengine ambao wapo salama, wataanza mazoezi Ijumaa kujiaandaa na mchezo wao dhidi ya Brighton.