Jumatatu , 19th Mar , 2018

Baada ya vigogo watatu wa soka nchini England kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la FA ambao ni Manchester United, Chelsea na Tottenham sasa mbio hizo zimegeuka vita kutokana mahitaji ya klabu hizo msimu huu.

Manchester United ambao ni mabingwa mara 12 wa kombe hilo, msimu huu ndio michuano pekee ambayo wanaweza kuwa mabingwa na watacheza nusu fainali na mabingwa mara 8 Tottenham Hotspurs ambao nao wanategemea kombe hilo pekee msimu huu.

Timu nyingine ambayo ipo kwenye vita ya kombe la FA ni Chelsea ambao ni mabingwa mara 7 wa kombe hilo watacheza na Southampton inayoshika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa EPL msimu huu.

Manchester United walitwaa kombe hilo kwa mara ya mwisho misimu miwili iliyopita chini ya Louis van Gaal huku Chelsea wakitwaa mara ya mwisho 2012. Tottenham wao walitwaa mara ya mwisho mwaka 1991. Mechi hizo zitachezwa 21-22 Aprili.

Katika msimamo wa ligi Manchester United inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 65 nyuma ya Man City yenye alama 81. Tottenham ipo katika nafasi ya 4 ikiwa na alama 61 wakati Chelsea ikiwa na alama 56 katika nafasi ya 5. Kimahesabu timu zote haziwezi tena kushindania ubingwa wa EPL huku pia zikiwa zimetolewa kwenye michuano ya UEFA.