Wacheza gofu 140 kutoka vilabu mbalimbali wachuana

Jumamosi , 16th Nov , 2019

Wachezaji 140 wa gofu kutoka vilabu mbalimbali  wameshiriki mashindano ya kombe la Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wacheaji katika viwanja vya Lugalo

Akizungumza kabla ya kuingia kucheza Jenerali mstaafu Waitara amesema, idadi hiyo ya wachezaji walioshiriki michuano ya kumuenzi, imempa faraja na kuona michuano hiyo inazidi kupata umaarufu hata nje ya nchi.

Licha ya hali ya hewa ya jiji la Dar es salaam kwa siku ya leo Novemba 16, 2019, kuwa na joto, lakini wachezaji wamefanikiwa kucheza na kumaliza viwanja 18.

Zaidi tazama Video hapo chini