Jumapili , 18th Mar , 2018

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema wachezaji wake walikuwa na hofu ya kucheza pamoja na ushindi waliopata dhidi ya Brighton kwenye Kombe la FA jana usiku.

"Hatukucheza kama nilivyotaka, wachezaji wanahofu na hawajacheza kama nilivyowaelekeza kucheza lakini tumepata ushindi kitu ambacho ni muhimu kuliko vyote", amesema.

Mabao ya Romelu Lukaku na Nemanja Matic yalitosha kuipa ushindi Man United na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA kwa mara ya 29 katika historia ya klabu hiyo.

Aidha Mourinho amesema wachezaji wake bado wanasumbuliwa na matokeo ya mechi iliyopita ambapo walitupwa nje ya michuano ya UEFA hatua ya 16 bora na Sevilla Jumanne ya wiki hii.

"Wakati mwingine wachezaji huathiriwa na kilichotokea uwanjani kwenye mchezo uliopita na madhara yake huja hadi kwenye mchezo husika na hicho ndio kinachanganya zaidi timu", ameongeza.