Jumamosi , 25th Jan , 2020

Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuwa wachezaji wake wawili iliowasajili kwenye dirisha dogo ambao ni Luis Miquissone na Shiza Kichuya, bado hawajapata kibali cha kimataifa (ITC) cha kuchezea klabu hiyo.

Kushoto ni Luis Miquissone

Taarifa ya Simba imeeleza kuwa,  'Luis Miquissone ITC yake bado haijafika, jambo hilo limeshafikishwa FIFA na linafanyiwa kazi'.

Aidha kuhusu Kichuya Simba imeeleza kuwa imefanya mawasiliano na klabu aliyokuwa akichezea ya Pharcos Misri.

Ramadhan Kichuya (kulia) akisaini mkataba

'Shiza Kichuya ITC yake bado haijafika klabu ya Pharcos ya Misri bado haijajibu maombi yetu ya kutuma ITC', imeeleza taarifa hiyo.