Waziri Mkuu atangaza neema kwa mashabiki wa mpira

Jumapili , 14th Apr , 2019

Watanzania wamejikuta wameangukiwa na neema katika Fainali za Vijana (AFCON) chini ya miaka 17, baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutangaza Watanzania wote kuingia uwanjani bure kuangalia mashindano hayo kuanzia kesho Jumatatu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye  ni mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa fainali za AFCON na alipopewa nafasi ya kuzungumza ndipo amesema, kuanzia kesho watanzania wote watapata uhuru wa kuingia uwanjani bure kwenda kuangalia fainali hizo.

Sisi kama serikali tunasema kuanzia kesho watanzania wote wataingia bure Uwanjani, Tanzania Oyee", amesema Waziri Mkuu.

Idadi ya ndogo ya mashabiki waliojitokeza uwanjani leo, inatajwa sababu ya Waziri Mkuu kutangaza kutokuwa na kiingilio ili kuongeza nguvu ya mashabiki uwanjani.