Jumamosi , 9th Oct , 2021

Klabu ya Yanga inatazamiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya JKU ya visiwani Zanzibar saa 1:00 usiku wa kesho Oktoba 10, 2021 kwenye dimba la Chamazi Jijini Dar es Salaam ili kujiweka fiti kabla ya michezo ya Ligi kuu  na mashidano mengine kurejea.

Kikosi cha Yanga cha msimu wa mwaka 2021-22.

li kushuhudia Wananchi wakishuka dimbani kucheza na wakali wa Zanzibar, JKU, Yanga imetangaza viingilio ni shilingi 3,000 kwa mzunguko na 5,00 kwa VIP A&B.

Kwa upande mwingine, Kocha wa viungo wa Yanga, HelmiGueldich amesema mashabiki wamtarajie  Yassin Mustapha kurejea dimbani siku za hivi karibuni baada ya kuanza mazoezi.

“Nadhani watu wamtarajie uwanjani Yassin hivi karibuni , ni kweli amekiwasha mazoezini na wenzake lakini bao hajawa fiti kiasi cha kucheza ndiyo maana tumewatengea mazoezi maalum yeye na Balama” Amesema Helmi.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC Tanzania akiwa na alama 6 baada ya ushindi wa michezo miwili dhidi ya Kagera Sukari na Geita Gold sawa na alama za kinara timu ya Polisi Tanzania inayoongoza kwa utofauti wa kufunga na kufungwa.