Ijumaa , 18th Oct , 2019

Uongozi wa Yanga umeweka wazi viingilio vitakavayotumika katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC na kufafanua sababu ya kupanga aina hiyo ya viingilio.

Makamu wa Rais wa Yanga na Afisa Habari

Mchezo huo utakaopigwa katika dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza, utakuwa na kiingilio cha Shilingi 10,000/= kwa mzunguko, shilingi 50,000/= kwa VIP na royal kwa shilingi 70,000/=.

Akizungumza sababu ya kuweka viingilio hivyo, Makamu Mwenyejiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na gharama halisi za kuandaa mchezo huo, ambapo makato makato pamoja na gharama mbalimbali zinahusika.

"Gharama za uwanja zinabakia zilezile, asilimia 10 zinaingia kwenye gharama za mchezo, zingine zinakwenda TFF, CAF, walinzi wa uwanja pamoja na gharama za tiketi", amesema Mwakalebela.

"Hatujaweka vigezo hivyo kwa ajili ya kupata faida bali ni kuhakikisha vitu vinafanyika, hata kama kuna 'zero gain' lakini iwepo katika bei ambazo kila mtu anaweza kuzimudu", ameongeza.

Aidha Mwakalebela amesema kuwa kikosi chake kiko swa kuelekea mchezo huo na wana uhakika wa kuibuka na ushindi katika uwanja wa nyumbani kwani malengo yao ni kutinga hatua ya makundi. Amewaomba mashabiki wa Yanga na Watanzania wapenda kandanda kuisapoti Yanga ili iweze kufanya vizuri na kuzirudisha pointi ambazo zitapelekea nchi kuingiza timu nne msimu ujao.

Yanga inatarajia kusafiri kesho, Oktoba 19 kuelekea Jijini Mwanza ambako itaweka kambi kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Pyramids utakaopigwa Oktoba 27.