Yanga kukutana na kisiki cha rekodi leo

Jumapili , 15th Mar , 2020

Mtanange mkali wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Namungo FC na Yanga unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa mkoani Lindi leo, ikiwa ni muendelezo wa ratiba ya ligi hiyo.

Namungo FC dhidi ya Yanga

Yanga inaingia katika mchezo huo ikitoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya KMC huku Namungo FC ikitoka sare ya bila kufungana na Biashara United.

Tangu Januari 29, 2020 ilipopoteza dhidi ya Simba SC, Namungo FC haijafungwa katika michezo 11 mfululizo ya ligi huku rekodi kubwa zaidi ni ile ya kupoteza mchezo mmoja pekee kati ya 13 iliyopita katika uwanja wake wa nyumbani, ikishinda mechi 9, sare 3 na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Coastal Union.

Katika msimamo wa ligi, Yanga inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 na Namungo FC ikiwa katika nafasi ya nne ya ligi na pointi zake 49.