Jumapili , 5th Jul , 2020

Katika mwendelezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, mabingwa wa ligi hiyo msimu huu Simba SC pamoja na Yanga ambao wanapigania nafasi ya pili, zitashuka dimbani kusaka pointi tatu.

Magolikipa wa Yanga wakiwa mazoezini

Michezo hiyo inachezwa nje ya Dar es salaam ambapo Simba wamesafiri hadi Mtwara kuwavaa Ndanda FC, huku Yanga wakisafiri hadi Musoma Mara kucheza na Biashara United.

Yanga wamesema mchezo huo ni wa kusaka pointi tatu muhimu hivyo hakuna namna zaidi ya kupata ushindi na makocha wametoa maelekezo kwa golikipa atayeanza kuhakikisha hakubali kufungwa.

Wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini

Agizo moja tu kwa makipa leo mazoezini, "Biashara United wasipate goli kwenye mchezo wetu". wameeleza Yanga.

Baada ya kutwaa ubingwa, Simba inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 79 kwenye mechi 32. Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 60 kwenye 32.