Wachezaji Mukoko Tonombe(Kushoto) ambaye ndiye mfungaji wa bao la Yanga leo akiwa na Tuisila Kisinda (Kulia) yeye ndiye aliyetoa pasi ya bao dhidi ya Kagera.
Katika mchezo huo bao la Yanga limefungwa na kiungo mkabaji raia wa Kongo Mukoko Tonombe katika Dakika ya 71 ya mchezo baada ya kuunganisha pasi Kutoka kwa winga Tuisila Kisinda.
Nahodha wa Yanga Deus kaseke amesema wamecheza na timu nzuri na timu hiyo ilikosa Bahati huku wao wakitumia nafasi waliyopata.
Ushindi huo ni wa sita mfululizo kwa Yanga dhidi ya Kagera katika Uwanja wa Kaitaba kama ambavyo reodi zinavyoonyesha tangu msimu wa 2015/16.
Yanga sc sasa inaongoza ligi baada ya kufikisha jumla ya pointi 7 baada ya kushuka dimbani mara 3 huku wakitarajia kucheza wiki ijayo dhidi ya Mtibwa sugar katika dimba Jamhuri Mjini Morogoro.
Katika mchezo mwingine uliopigwa mapema leo huko mkoani Rukwa, Tanzania Prisons imepata ushindi wake wa kwanza wa VPL kwa kuinyuka Namungo bao 1-0 .