Jumatano , 12th Aug , 2020

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Faridi Mussa kwa mkataba wa miaka miwili.

Mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Azam, Farid Mussa (Kushoto Pichani), akisaini Mkataba mbele ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said (Kulia pichani)

Faridi Mussa anajiunga na mabingwa wa kihistoria wa Tanzania akiwa mchezaji huru akitokea katika klabu ya CD Tenerife ya Hispania.

Yanga imekamilisha usajili wa nane katika dirisha la usajili linaloendelea ikiwa katika harakati za kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa mashindano.

Nyota huyo alijiunga na Teneriffe ya Hispania mwaka 2016 akitokea Azam Fc na amesaini Yanga akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu hiyo ya Hispania kumalizika.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga katika dirisha hili la usajili ni pamoja na Waziri Junior, Bakari Nondo Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu Ninja, Zawadi Mauya, Yassin Mustapha, na Yacoub Sogne.