Yanga yamtolea uvivu Bernard Morrison

Jumatano , 24th Jun , 2020

Klabu ya Yanga imempiga faini ya shilingi Mil 1,500,000 mchezaji Bernard Morrison kwa kosa la kuongea na vyombo vya habari kambini, bila kufuata kanuni za klabu.

Barnard Morrison

Katika taarifa iliyotolewa kwa umma leo, Yanga imesema kuwa jambo hilo ni kuhujumu na kukiuka taratibu na kanuni za klabu huku akiwa na nia ovu.

Pia kuhusiana na suala la mkataba wa klabu na mchezaji huyo, Yanga imesema kuwa Januari 15, 2020 klabu iliingia mkataba na Morrison wa kuitumikia klabu hadi Julai 14, 2022 na kwamba hivi sasa ni mali yao.

Soma taarifa kamili ya klabu hapa chini.