Yanga yazungumzia kutoswa na Gadiel Michael

Jumanne , 9th Jul , 2019

Uongozi wa Yanga umezungumza kwa mara ya kwanza kufuatia kuondoka kwa mlinzi wake kisiki, Gadiel Michael ambaye ametimkia kwa mahasimu wao Simba.

Gadiel Michael

Gadiel Michael ametambulishwa hii leo na klabu ya Simba kuwa mchezaji wake rasmi kwa mkataba wa miaka miwili.

Uongozi wa Yanga kupitia kwa Meneja wake, Hafidh Saleh umesema kuwa wao kama klabu wameshamsahau Gadiel kwakuwa wameshasajili wachezaji bora kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara.

"Gadiel Michael alikuwa mchezaji wetu, amemaliza kandarasi yake na hakupenda kuongeza mkataba ameamua kuondoka, kwahiyo kuna maisha mengine. Sisi tumeshamsahau ni kama historia kwetu", amesema Hafidh Saleh.

Pia Hafidh amezungumzia maandalizi kamili ya kikosi cha Yanga kuelekea ufunguzi wa ligi mwishoni mwa mwezi ujao, ambapo amesema kikosi kamili pamoja na kocha Zahera watawasili wiki ijayo.

Tazama video hapa chini akizungumza zaidi.