Jumatatu , 11th Mar , 2019

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera baada ya mchezo wa jana dhidi ya KMC ambapo Yanga ilishinda mabao 2-1, ameaga kuwa anaondoka nchini kuelekea kwao DR Congo.

Kocha Mwinyi Zahera akiwa na wachezaji wa Yanga.

Zahera anakwenda DR Congo kwaajili ya majukumu ya timu ya taifa ambayo yeye ni kocha msaidizi huku akisisitiza kuwa taifa lake lina mchezo mgumu sana dhidi ya Liberia kuwania kufuzu AFCON 2019.

''Naenda Congo, tupo na mechi ngumu sana, nisiulizwe chochote kuhusu Simba au Yanga nawaachia namba ya kocha msaidizi Noel Mwadila mtamuuliza yote mimi sitamjibu hata mtu mmoja'', amesema.

Zahera anaondoka nchini kesho Jumanne Machi 3, 2019, lakini hajaweka wazi kama anaondoka na mshambuliaji Heritier Makambo ambaye alitajwa katika kikosi cha wachezaji 40 wa awali kuelekea mchezo huo.

DR Congo ipo kundi G ambalo linaongozwa na Zimbabwe yenye pointi 8, Liberia yenye pointi 7 huku DR Congo wakiwa na pointi 6 wakati Congo Brazzaville wakiwa na pointi 5.