Jumatano , 20th Feb , 2019

Aliyewahi kuwa msemaji wa klabu ya Yanga ambaye hivi sasa ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amesema uwepo wa kocha Mwinyi Zahera ndani ya Yanga umesaidia tu kuhamasisha mashabiki wachangie timu.

Kocha Mwinyi Zahera (katikati).

Muro ameyasema hayo jana jioni jijini Arusha kwenye mchezo wa African Lyon dhidi ya Simba, ambapo aliweka wazi kuwa Zahera sio kocha anayejua wachezaji bali ni mhamasishaji tu.

''Ngassa sio mchezaji wa kucheza Yanga kwasasa aende akawe akasome ukocha afundishe timu za vijana, hata Boban naye mwili na akili vimeshakataa, kwahiyo kocha huyo abaki tu kuwa mhamasishaji wa michango lakini kuhusu kujua wachezaji hawajui'', alinukuliwa akisema.

Aisha Muro aliweka wazi kuwa kinachotakiwa ni Yanga kujua thamani yake na ifike muda irejee kwenye misingi yake tofauti na ilivyosasa.

Katika mchezo huo wa jana ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, Muro alionekana na swahiba wake Haji Manara ambaye waliwahi kuwa washindani wakubwa wakai Muro bado yupo Yanga. Pia Haji Manara alimvalisha Muro jezi ya Simba.