Jumatatu , 18th Feb , 2019

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane amezidi kuitamanisha klabu ya Chelsea ambayo kwa mujibu wa tetesi mbalimbali inatafuta kocha mbadala wa Maurizio Sarri anayenukia kutimuliwa Stamford Bridge.

Zinedine Zidane

Tetesi kutoka mtandao wa BBC Sports, Zidane ametoa sharti la kupewa Pauni 200m za usajili ili aweze kuifundisha klabu hiyo.

Pia sharti lingine alilolitoa ni pamoja na kuhakikishiwa kuwa nyota wa klabu hiyo, Mbelgiji, Eden Hazard anapewa mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Zidane amekuwa nje ya uwanja tangu mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuisaidia Real Madrid kushinda Klabu Bingwa Ulaya mara tatu mfululizo na Klabu Bingwa ya Dunia.

Kocha Maurizio Sarri amekuwa na shinikizo katika klabu yake, juu ya matokeo yasiyoridhisha anayoyapata, ikiwemo kichapo kizito cha mabao 6-0 kutoka kwa Manchester City akatika mchezo wa EPL mwanzoni mwa mwezi Februari.

Katika miaka ya karibuni, Chelsea haijawahi kukaa na makocha wake kwa misimu mitatu mfululizo, ambapo tangu Jose Mourinho alipojiunga na klabu hiyo msimu wa 2003/04, jumla ya makocha 8 wamepita klabuni hapo.