Zidane apewa listi ya 'mastaa' wa kutua Madrid

Jumanne , 12th Mar , 2019

Baada ya kocha Zinedine Zidane kurejea rasmi klabu ya Real Madrid kwa mtakaba wa miaka mitatu, Rais wa klabu amempa listi ya wachezaji wa kuanza nao katika usajili wa msimu ujao.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez (kushoto) akiwa na kocha Zinedine Zidane.

Akizungumza katika hali ya utani wakati wa utambulisho wa Zidane, Rais wa klabu, Florentino Perez amesema ana matumaini kuwa Zidane atakuwa ni daraja la kuwapata mstaa wa PSG, Kylian Mbappe na Neymar.

"Zidane ni Mfaransa, kwahiyo anaweza kufanya kitu fulani na Mbappe", amesema Perez na alipoulizwa ni nani atamchagua kumsajili kati ya Neymar na Mbappe, Perez akajibu "wote".

Real Madrid ilifikia uamuzi wa kumuondoa kocha, Santiago Solari kufuatia mlolongo wa kusuasua katika michuano mbalimbali, ambapo mpaka anaondoka, Real Madrid ilikua imesalia katika La Liga pekee ambapo inakamata nafasi ya tatu huku ikiondoshwa katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya na Copa del Rey.

Urejeo wa Zidane unaaminika kuwa unaweza kuwa sababu ya kuwavuta mastaa kutoka vilabu vikubwa barani Ulaya ambao wamekuwa wakihusishwa kujiunga na miamba hiyo, ni kwa sababu ya uhodari wa kocha huyo kuishi na wachezaji wake..

Licha ya Kylian Mbappe, mstaa wengine wanaohusishwa kujiunga na Real Madrid ni pamoja na Neymar, Eden Hazard, Christian Eriksen na Harry Kane.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.