Jumatano , 19th Jun , 2019

Hivi sasa tunahesabu masaa takribani 48 kabla ya michuano mikubwa zaidi barani Afrika (AFCON) kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali nchini Misri.

Mshindi wa taji la AFCON 2017, Cameroon

Michuano ya mwaka huu itashirikisha timu 14, ikiwa ni ongezeko la timu nane kutoka 16 zilizoshiriki michuano iliyopita.

Zipo timu kadhaa ambazo zinapewa nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hiyo, ikiwemo Misri, Algeria, Senegal, Morocco na Ghana. Lakini huenda ukawa hufahamu kuwa kuna mataifa ambayo yaliwahi kutikisa soka la Afrika na kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.

Hizi hapa ni timu ambazo zinashikilia rekodi ya kushinda ubingwa wa michuano hiyo mpaka sasa, zikiongozwa na Misri ambayo imeshinda mara 7, ikifuatiwa na Cameroon ambayo imeshinda ubingwa mara 5.

Timu zingine ambazo zimeshinda michuano ni, Ghana (4), Nigeria (3), Ivory Coast (2), Congo DR (2). Timu ambazo zimeshinda ubingwa huo mara moja ni pamoja na Sudan, Tunisia, Morocco, Ethiopia, Congo, Afrika Kusini, Algeria na Zambia.

Ikumbukwe kuwa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ipo katika kundi C kwenye michuano hiyo, pamoja na timu za Kenya, Algeria na Senegal