
Kocha mpya wa Simba Zoran Maki
Zoran amesema amechukua ubingwa nchini Algeria na CR Belouzdad na ameshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Shirikisho hivyo anaamini anaweza kufanya hivyo akiwa hapa.
'' Maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi Zoran amesema itamtosha kukiandaa kikosi na kurejesha ubora wake wa kupambania mataji''amesema Zoran
Kuhusu usajili Zoran amesema ameshirikishwa katika kusajili wachezaji wapya na anaamini tutakuwa na timu imara yenye kuleta ushindani ndani na michuano ya Afrika.
“Simba ni timu kubwa ina mashabiki wengi. Nina uzoefu wa mazingira ya Afrika, hata huu muda wa mwaka mmoja naweza kufanya mambo makubwa,” amesema Zoran