
Katibu Mwenezi wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu.
basi yeye atahama ACT Wazalendo na kuhamia CCM.
Ado ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa 'twitter' wakati akijibizana na Dkt. Mollel, ambapo www.eatv.tv, ilipomtafuta Ado ili kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake ambapo alidai hana mpango huo ila alimjibu vile Mollel kwakuwa alijua hana uwezo wa kuthibitisha.
"Sina mpango wa kuhamia CCM. Nimempa changamoto Dk. Mollel kwa sababu najua hana ubavu wa kuthibitisha. Amekurupuka tuu ili apate kiki kupitia Zitto ili na yeye apate kusikika. Angekuwa msomi kweli angekwenda kutazama mapato ya Zanzibar kwa mwaka husika kisha angejua anachoongea hakipo", amesema Ado.
Ameongeza kuwa, "Mimi si mhasibu na sikuwepo kwenye kikao cha kamati ya PAC. Lakini nakuhakikishia Dk. ukinithibitishia kwamba CAG kasema fedha yote 1.5T ni hela ya Zanzibar iliyoonekana kwenye mahesabu ya TRA basi nitajiuzulu uenezi wa ACT-Wazalendo kesho na kuchukua kadi ya CCM".
Hayo yamejiri baada ya Dk. Mollel kuonekana kumshambulia Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, kupitia mtandao wake wa Twitter aliporipoti hoja ya 1.5 Trilioni kupelekwa rasmi kwenye kamati ya PAC.
"Mh zitto Natumai sasa utaacha kimbelembele, CAG kakuumbua kuwa ulikuwa unasema uongo , amekuonyesha kuwa 1.5T ni fedha iliokusanywa Zanzibar na inatumika Zanzibar na haijaja bara ila imeonyeshwa tu kwenye ripoti za TRA", ameandika Dk. Mollel.