Alhamisi , 19th Dec , 2019

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula, amewataka vijana, kuachana na fikra na dhana ya kuajiriwa badala yake wajenge tabia ya kujiajiri na kuanzisha miradi itakayozalisha ajira kwa wengine.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula.

Mangula ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa Chuo cha Uongozi na mafunzo cha Ihemi mkoani Iringa, ambapo amesema wasomi wanaohitimu vyuo mbalimbali nchini, wasifikirie kuajiriwa bali wajiajiri.

"Mafunzo mmeshapewa na yatakuwa yanahusika na Ujasiriamali, ili muondoe dhana ya kuwa kuna kuajiriwa, hasa kwenu nyinyi vijana ambao mtapitia kwenye chuo hiki cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi" amesema Mangula.

Tazama video kamili hapo chini.