Baraza la madiwani kumfukuza mfanyakazi mtoro
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Mbinga limeazimia kumfukuza kazi mfanyakazi mmoja wa halmashauri hiyo kwa kosa la utoro kazini huku likiwapeleka kwenye kamati ya maadili wafanyakazi watatu wa halmashauri hiyo wakiwa na makosa hayo hayo ya utoro katika vituo vyao vya kazi.

